1Nimekuja kwenye bustani yangu, dada yangu,bibi arusi wangu;nimekusanya manemane yangu pamojana kikolezo changu.Nimekula sega langu la asali na asali yangu;nimekunywa divai yangu na maziwa yangu.MarafikiKuleni, enyi marafiki, mnywe;
kunyweni ya kutosha, ee wapenzi.
2Nililala lakini moyo wangu ulikuwa macho.
Sikiliza! Mpenzi wangu anabisha:“Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu,
hua wangu, asiye na hitilafu.Kichwa changu kimeloa umande,na nywele zangu manyunyu ya usiku.”
3Nimevua joho langu:je, ni lazima nivae tena?Nimenawa miguu yangu:je, ni lazima niichafue tena?
4Mpenzi wangu aliweka mkono wake kwenye tundu la komeo;moyo wangu ulianza kugonga kwa ajili yake.
5Niliinuka kumfungulia mpenzi wangu,mikono yangu ikidondosha manemane,vidole vyangu vikitiririka manemane,penye vipini vya komeo.
6Nilimfungulia mpenzi wangu,lakini mpenzi wangu alishaondoka;
alikuwa amekwenda zake.Moyo wangu ulishuka kwa kuondoka kwake.Nilimtafuta lakini sikumpata.
Nilimwita lakini hakunijibu.
7Walinzi walinikutawalipokuwa wakifanya zamu za ulinzi mjini.Walinipiga, wakanijeruhi,wakaninyangʼanya joho langu,
hao walinzi wa kuta!
8Enyi binti za Yerusalemu, ninawaagiza:kama mkimpata mpenzi wangu,mtamwambia nini?Mwambieni ninazimia kwa mapenzi.
9Je, mpendwa wako ni bora kuliko wengine namna gani,wewe uliye mzuri kupita wanawake wote?Je, mpendwa wako ni mzuri kuliko wengine, namna gani,hata unatuagiza hivyo?
10Mpenzi wangu anangʼaa, tena ni mwekundu,wa kuvutia miongoni mwa wanaume kumi elfu.
11Kichwa chake ni dhahabu safi kuliko zote,nywele zake ni za mawimbi
na ni nyeusi kama kunguru.
12Macho yake ni kama ya huakandokando ya vijito vya maji,aliyeogeshwa kwenye maziwa,yaliyopangwa kama vito vya thamani.
13Mashavu yake ni kama matuta ya vikolezoyakitoa manukato.Midomo yake ni kama yungiyungiinayodondosha manemane.
14Mikono yake ni fimbo za dhahabuiliyopambwa kwa krisolitho.Mwili wake ni kama pembe ya ndovu iliyongʼarishwailiyopambwa na yakuti samawi.
15Miguu yake ni nguzo za marmarzilizosimikwa katika vitako vya dhahabu safi.Sura yake ni kama Lebanoni,bora kama miti yake ya mierezi.
16Kinywa chake chenyewe ni utamu,kwa ujumla yeye ni wa kupendeza.Huyu ndiye mpenzi wangu, huyu ndiye rafiki yangu,ee binti za Yerusalemu.