Inapakia...
šŸ“–

Biblia Takatifu

BiblicaĀ® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifuā„¢
BIB • 13 mistari

Wimbo Ulio Bora 6

Wimbo Ulio Bora • Sura 6 / 8

1Mpenzi wako amekwenda wapi,ewe mzuri kupita wanawake wote?Mpenzi wako amegeukia njia ipi,tupate kumtafuta pamoja nawe?

2Mpenzi wangu amekwenda bustanini mwake,kwenye vitalu vya vikolezo,kujilisha bustaninina kukusanya yungiyungi.

3Mimi ni wake mpenzi wangu,na mpenzi wangu ni wangu;
yeye hujilisha katikati ya yungiyungi.

Shairi La Tano

4Wewe ni mzuri, mpenzi wangu, kama Tirsa,upendezaye kama Yerusalemu,
umetukuka kama jeshi lenye bendera.

5Uyageuze macho yako mbali nami,yananigharikisha.Nywele zako ni kama kundi la mbuziwanaoteremka kutoka Gileadi.

6Meno yako ni kama kundi la kondoowatokao kuogeshwa.Kila mmoja ana pacha lake,hakuna hata mmoja aliye peke yake.

7Mashavu yako nyuma ya shela yakoni kama vipande viwili vya komamanga.

8Panaweza kuwepo malkia sitini,masuria themanini
na mabikira wasiohesabika;

9lakini hua wangu, mkamilifu wangu,ni wa namna ya pekee,binti pekee kwa mama yake,kipenzi cha yeye aliyemzaa.Wanawali walimwona na kumwita aliyebarikiwa;malkia na masuria walimsifu.

10Ni nani huyu atokeaye kama mapambazuko,mzuri kama mwezi, mwangavu kama jua,
ametukuka kama nyota zifuatanazo?

11Niliteremka kwenye bustani ya miti ya miloziili kutazama machipuko ya bondeni,kuona kama mizabibu imechipuaau kama mikomamanga imechanua maua.

12Kabla sijangʼamua,shauku yangu iliniweka
katikati ya magari ya kifalme ya kukokotwa na farasi ya watu wangu.

13Rudi, rudi, ee Mshulami;rudi, rudi ili tupate kukutazama!MpenziKwa nini kumtazama Mshulami,kama kutazama ngoma ya Mahanaimu?*

Tanbihi

*

Mahanaimu hapa ina maana ya majeshi mawili.