Inapakia...
📖

Biblia Takatifu

Biblica® Toleo Wazi Neno: Bibilia Takatifu™
BIB 8 mistari

Zaburi 129

Zaburi • Sura 129 / 150

Maombi Dhidi Ya Adui Za Israeli
Wimbo wa kwenda juu.

1Wamenionea mno tangu ujana wangu;Israeli na aseme sasa:

2wamenionea mno tangu ujana wangu,lakini bado hawajanishinda.

3Wakulima wamelima mgongo wangu,na kufanya mifereji yao mirefu.

4Lakini Bwana ni mwenye haki;amenifungua toka kamba za waovu.

5Wale wote waichukiao Sayunina warudishwe nyuma kwa aibu.

6Wawe kama majani juu ya paa,ambayo hunyauka kabla hayajakua;

7kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake,wala akusanyaye kujaza mikono yake.

8Wale wapitao karibu na wasiseme,“Baraka ya Bwana iwe juu yako;
tunakubariki katika jina la Bwana.”